Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya
Mkusanyiko wa picha bora kutoka Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii:
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Nchini Liberia, mjini Monrovia, mpiga baragumu huyu anaonekana akipiga baragumu kwa furaha wakati wa sherehe ya kumuapisha nyota wa zamani wa soka George Weah kuwa rais mpya wa nchi hiyo uwanja wa Samuel Kanyon Doe 22 Januari.
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Mvulana nchini Zimbabwe anywa maji kutoka kwenye mfereji katika kisima eneo la Chegutu, 100km magharibi mwa mji mkuu Harare siku ya Jumatatu.
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Siku iliyofuata, mzoga wa samaki unaonekana katika bwawa la Theewaterskloof lililokauka Afrika Kusini katika mkoa wa Cape Magharibi ambao umekabiliwa na ukame kwa muda mrefu.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa huko hakuna wasiwasi wa uhaba wa maji. Hapa, mvulana mtumishi wa kanisa anaonekana akiwanyunyizia waumini maji yaliyobarikiwa katika kanisa moja la Kiothodoksi mjini Addis Ababa. Ilikuwa ni Ijumaa wakati wa sherehe ya kubatizwa kwa Yesu katika mto Jordan ambayo hufahamika kama Timket.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Wasichana watumishi kanisani pia wanaonekana hapa wakihudhuria ibada hiyo ya Timket...
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Wavulana hawa pia hawakuachwa nyuma.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Siku tatu baadaye Januari 22, katika jiji la Herzliya nchini Israel, wahamiaji kutoka Afrika wanaandamana dhidi ya uamuzi wa serikali wa kuwahamisha kwa lazima maelfu ya wahamiaji wa Afrika waliofika nchini humo.
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Siku hiyo pia, mwanamke anatungika vitambaa vilivyopakwa rangi katika mji wa Abidjan, Ivory Coast. Serikali nchini humo inapanga kutumia sekta ya nguo na mavazi kuunda nafasi zaidi za ajira.
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Na raia hawa wa Ghana wanaoishi na ulemavu wanaonekana hapa wakishindana katika mashindano ya soka ya kuteleza yalitoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka ya Kuteleza mjini Accra, Ghana.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Mjini Lome, Togo Jumamosi, mwanamume huyu aliyepakwa rangi mwilini, rangi za bendera ya taifa hilo, anashiriki maandamano ya kushinikiza familia ya Eyadema ambayo imetawala nchi hiyo kwa miaka 50 kuondoka madarakani.
Haki miliki ya pichaEPAImage caption
Na jijini Nairobi siku ya Jumanne, wanawake hawa wenye bango la kulalamikia tuhuma za kubakwa kwa wanawake waliojifungua watoto Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wanaonekana wakiwa wamejilaza chini.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Ijumaa, wanafunzi hawa wawili walikuwa miongoni mwa wengine 14,000 waliofuzu wakati wa mahafali katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Haki miliki ya pichaReutersImage caption
Mjini Cairo, Misri siku ya Alhamisi, sanamu ya karibu miaka 3,000 ya Mfalme Ramses II nayo ilihamishwa kutoka uwanja uliopewa jina lake hadi kwenye makavazi kuihifadhi isiharibiwe na jua na mvua.