Miguel Díaz-Canel aapishwa kama rais mpya wa Cuba

Cuba power Haki miliki ya picha AFP
Image caption Miguel Díaz-Canel mwenye shati jeupe

Miguel Díaz-Canel ameapishwa rasmi kama rais mpya wa Cuba na kuichukuwa nafasi ya Raúl Castro aliyerithi uongozi kutoka kwa kakake aliyekuwa mgonjwa Fidel mnamo 2006.

Ni mara ya kwanza tangu mapinduzi ya 1959 kuchaguliwa kiongozi mkuu wa serikali ya nchi hiyo asiyetoka familia ya Castro.

Díaz-Canel alikuwa anahudumu kama makamu wa kwanza wa rais kwa miaka mitano iliyopita.

Licha ya kwamba Bwana Díaz-Canel alizaliwa baada ya mapinduzi, yeye ni mfuasi mkali wa Raúl Castro na hatarajiwi kufanya mageuzi yoyote makali.

Alichaguliwa na wabunge, wote 605 waliochaguliwa mwezi Machi baada ya kusimama bila ya upinzani.

Bwana Castro anatarajiwa kuendelea kuwana ushawishi wa kisiasa nchini katika wadhifa wake wa kiongozi wa chaa tawala cha kikomyunisti Cuba.

Miguel Díaz-Canel ni nani?

Miguel Díaz-Canel, ana miaka hamsini na mitano, ambaye kwa taaluma ni mhandisi wa zamani.

Bwana Diaz-Canel huonekana kama huria kijamii na mbobevu wa teknolojia mpya ingawa hatazamiwi kumaliza mfumo wa chama kimoja nchini humo, ingawa ni mapema mno kumuweka katika nafasi ya namna hiyo kwa sasa.

Huwezi kusikiliza tena
Fidel Castro, kiongozi aliyekuwa mwiba kwa Marekani

Kwa tabia Miguel ni kiongozi mnyofu na tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa kuwa makamu wa raisi wa baraza la Congress la Cuba mnamo mwaka 2013 ingawa tangu wakati huo amekuwa ni mtu wa karibu wa bwana Castro.

Kwa miaka mitano iliyopita, amekuwa akiandaliwa kushika hatamu za uongozi katika nafasi ya raisi na kupokea madaraka, Ingawa hata kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa makamu wa raisi, amekuwa ni mwanasiasa mkongwe .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Díaz-Canel anafahamika kama mtu wa watu

Alizaliwa mnamo mwezi wa nne mwaka 1960, mwaka mmoja baada ya Fidel Castro alipokula kiapo cha kushika nafasi ya waziri mkuu.

Miguel Díaz-Canel alisomea masuala ya uhandisi wa umeme na kuanza na kuanza harakati za kisiasa mapema akiwa na miaka 20 kama mwanachama wa chama cha Kikomunisti huko Santa Clara.

Alipokuwa akifundisha uhandisi katika chuo kikuu, Raúl Castro alimsifu kwa "uaminifu wa kiitikadi".

Makabidhiano haya ya madaraka yanahitimisha miongo sita ya utawala wa Castro na ndugu yake marehemu Fidel, ambaye aliongoza mapinduzi ya mwaka 1959.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii