Burger ya mboga inayotoa damu inapokatwa
Huwezi kusikiliza tena

Habari za Global Newsbeat 1500 24/04/2018

Viwanda vya kutengeneza nyama vinakisiwa kuchangia pakubwa katika utoaji wa gesi mbaya. Kampuni ya teknologia ya Sillicon Valley inasema utumiaji wa mboga zilizopandwa katika maabara zaweza kupunguza ulaji wa nyama. Mfano ni mboga inayofanana na kunuka kama nyama lakini ni mboga. Je, mboga kama hii yaweza kukushawisha uwache kula nyama. Sema nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook, bbcSwahili.