Israel yafutilia mbali mpango wa kuwatimua wahamiaji Waafrika

Waandamanji Israel dhidi ya mpango wa kuwahamisha kwa lazima Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Htama ya wahamiaji wa Afrika imezusha mzozo mkubwa

Israel imefutilia mbali mpango wa kuwatimua kwa lazima maelfu ya wahamiaji haramu wa kutoka Afrika.

Katika barua iliyoiandikia mahakama ya juu zaidi ya Israel, serikali imesema kwamba kuwatimua kwa lazima wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika, "sio suala kuu katika ajenda".

Hatahivyo, maafisa wa uhamiaji wa Israel bado wanatafuta njia za kuwahamisha wahamiaji hao kwa hiari, ilisema barua hiyo.

Htamaya wahamiaji haramu takriban 30,000 kutoka mataifa ya Afrika imekuwa ni suala linalozuhs amzozo mkubwa.

Mahakam ya juu zaidi nchini humo awali ilisitisha mipango ya kuwahamisha wahamiaji hao - wengi wao kutoka Eritrea na Sudan - ila iwapo watakubali kwa hiari kupokea kitita cha fedha na tiketi ya ndege kutoka Israel.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu baada ya hpo aliafutilia mbali makubaliano na Umoja wa mataifa kuwatafutia makaazi wahamiaji hao katika mataifa ya magharibi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameshutumiwa nyumbani na kimataifa kuhusu suala hilo

Chini ya makubaliano hayo, Israel ilistahili kutoa makaazi ya muda kwa mhamiaji Israel kwa kila mhamiaji anayetafutiwa makaazi ng'ambo.

Siku ya Jumatatu, Wanachama 18 wa Democratic katika bunge la wawakilishi inaarifiwa wamemuandikia Netanyahu barua wakimuambia kwamba 'wameshangazwa' na 'kuvunjwa moyo' na hatua yake kufutilia pendekezo hilo la Umoja wa mataifa wakieleza kuwa iliwaacha wahamiaji katika njia panda na bila ya muelekeo wa 'hatua inayofuata'.

Wahamiaji wanatoka wapi?

Baadhi ya wahamiaji wa Afrika nchini Israel wanatoka Eritrea - taifa la chama kimoja ambalo viongozi wake wameshutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binaadamu na jopo la uchunguzi la Umoja wa mataifa na taifa la Sudan lililoathirika na vita.

Wanasema wametoroka hatari nyumbani na kwamba sio salama kwao kurudi katika nchi nyingine ya Afrika, lakini Israel inatizama baadhi ya watafuta hifadhi hao wa Afrika kuwa wahamiaji wa kiuchumi.

Wengi wao waliwasili kutoka Misri miaka kadhaa nyuma, kabla ya ukuta mpya kujengwa katika mpaka jangwani.

Hili limesitisha kwa kiwango kikubwa uhamiaji huo haramu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wa kutoka Afrika katika kituo cha kizuizi kusini mwa Israel

Suala hili linazusha mzozo kiasi gani?

Uamuzi uliopitishwa Januari kuwapa wahamiaji kitita cha pesa na tiketi ya ndege kutoka Israel kwa hiari au kwa namna nyingine kwa kushurutishwa umeshutumiwa Israel.

Baadhi ya wakosoaji nchini na kwa baadhi ya jamii ya wayahudi walioko ng'amb o - wakiwemo mabalozi wa zamani na manusura ya mauaji ya kimbari - Holocaust - wanasema mpango huo hauna maadili na ni doa katika sura ya kimataifa ya taifa hilo.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi limesema hatua hiyo inakiuka sheria za nchini na kimataifa na kulishuhudiwa maandamano makubwa Israel.

Netanyahu amesema kupingwa kwa hatua hiyo ni upuuzi mtupu usiokuwa na msingi na kwamba Israel itawapa hifadhi "wakimbizi wa kweli".

Hatahivyo, wanaharakati wamegusia kwamba ni wahamiaji wachache tu kutoka Eritrea na Sudan waliotambuliwa kama wakimbizi nchini Israel tangu nchi hiyo ipokee jukumu la kushughulikia maombi ya wahamiaji kutoka kwa Umoja wa mataifa mnamo 2009.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii