Wakenya waliotaka miili yao kuchomwa baada ya kufariki

Tanuru zinazotumiwa kuchoma wafu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tanuru zinazotumiwa kuchoma wafu

Mwanasiasa na mpiganiaji wa vyama vingi Kenneth Matiba ambaye mwili wake utachomwa siku ya Ijumaa anajiunga na orodha ya watu maarufu nchini Kenya ambao wametaka kutozikwa kulingana na tamaduni nchini Kenya.

Mwili wa mwanasiasa huyo ambaye amesifiwa kama mpiganiaji wa uhuru wa pili utachomwa katika makaburi ya Langata siku ya Ijumaa, kulingana na matakwa yake, familia imesema.

Na katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wanasiasa, viongozi wa makanisa na wanamichezo maarufu pia wameamua kuchagua njia hiyo wengine wakienda kinyume na matakwa ya familia zao na jamii.

Askofu wa zamani wa kanisa la Anglikana alianzisha mjadala kuhusu kifo katika kanisa hilo ambalo aliloliongoza na miongoni mwa Wakenya 2005, mwili wake ulichomwa kulingana na na kile ambacho familia yake inasema ni wasia wake.

Miaka mitatu awali mwili wa mkewe Mary Kuria ulikuwa umechomwa. Mwili wa bi Mary Nyambura Kuria ulichomwa na kuwa majivu katika eneo la Lang'ata siku mbili tu baada ya kufariki katika hospitali ya Nairobi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jumba la tanuru

Kila uchao idadi ya watu wanaoamua kuteketezwa moto wanapofariki inaongezeka ikilinganishwa na wanaoamua miili yao izikwe.

Kuna sababu nyingi zinazochangia uamuzi huo:

Gharama: Kwa jumla gharama ya kuchomwa ni chini ya ile ya kuzikwa. Huhitaji kaburi katika kuchoma maiti wala jiwe la kaburini , na vifaa vinavyotumika katika kuteketeza maiti ni vya bei rahisi ikilinganishwa na kuzika katika majeneza. Nchini Kenya gharama ya kuchoma maiti ni kati ya dola 1000 - 2200.

Nafasi za makaburi: Suala la nafasi za makaburi au ardhi wanakozikwa maiti ni changamoto kubwa hususan katika maenoe ya miji . Kuna ardhi kidogo sana za kuzika na jamii huwana wasiwasi kuuza ardhi zao kwa minajili ya kugeuza kuwa eneo la kuzika maiti.

Ni njia rahisi: Kuchoma maiti kunaondosha wasiwasi na kero za kutafuta ardhi, majeneza kuandaa mazishi, kama kutafuta wabeba Jeneza, tofuati na kuchoma mwili ambapo majivu ya mwisho huhifadhiwa katika jagi dogo ambalo ni rahisi kulibeba kwa mkono.

Wasiwasi wa kimazingira: Kwa kawaida kemikali hutumiwa katika kutayarisha mwili uzikwe ardhini. Kweli huwa kuna hewa mkaa/chafu nyingi mwili unapochomwa lakini kadri teknolojia inavyoendelea kukuwana vifaa kuboreshwa, athari kwa mazingira inaongezeka. Hatahivyo bado kuna mjadala, lakini kwa jumla inaonekana ni bora kwa mazingira kuchoma kuliko kuzika maiti.

Tamaduni na imani: Tamaduni na imani za jamii ni muhimu na baadhi ya imani kama Wahindu ni sharti maiti achomwe. Kwa wengine familia huamua kumuaga mtu anapofariki kwa njia ya ki aina yake.

Watu maarufu Kenya waliochomwa baada ya kufariki

Image caption Eneo la kuchoma maiti
  • Manasses Kuria

Habari za kuchomwa kwake zilijiri bila kutarajiwa kwa waombolezaji ambao walikutana katika kanisa la All Saints Cathedral mjini Nairobi kwa hafla ya kutoa shukrani.

Uamuzi huo ulisababisha mjadala katika kanisa hilo kuhusu uchomaji wa miili , huku wanachama wengi wakipinga wazo hilo.

  • Peter Habenga Okondo

Muongo mmoja uliopita, aliyekuwa waziri wa KANU Peter Okondo pia alikuwa amechomwa katika zoezi ambalo lilizua migawanyiko kati ya familia ya waziri na jamii yake ya Banyala.

Idadi kubwa ya wanakijiji waliwasili mjini Nairobi kabla ya kugundua kwamba mkewe alikuwa tayari ameuchoma mwili wake

  • Joshua Okuthe

Tatizo kama hilo lilionekana kufuatia kuchomwa kwa mwili wa msimamizi wa michezo wa zamani Joshua Okuthe. Mkewe wa kwanza Ruth Florence aliuchoma mwili wa mumewe mwenye umri wa miaka 62 mnamo mwezi Julai 9 2009 katika makaburi ya kariokor siku nne baada ya kifo chake.

Familia yake ililazimika kuzika jeneza tupu nyuma ya chumba chake cha kulala mjini Tamu, Wilaya ya Muhoroni kwa kuwa alitaka achomwe kulingana na wasia wake.

  • Wangari Maathai
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wangari Maathai

Mshindi wa tuzo ya Nobel marehemu Wangari Maathai alichomwa 2011 katika sherehe kubwa iliofanywa katika faragha za tanuru ya Kariokoo.

Familia ya mwanamazingira huyo na serikali zilikubali kuuchoma mwili huo kabla ya mabaki yake kuhifadhiwa katika Taasisi ya Wangari Maathai kuhusu amani na utafiti wa mazingira, kulingana na matakwa yake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii