Bango lililoandikwa kwa Kichina Nairobi lazua mdahalo

Tangazo lenyewe Haki miliki ya picha HISANI

Bango la matangazo ambalo lilikuwa limeandikwa kwa Kichina na kuweka katika barabara kuu ya Mombasa kwenda Nairobi limeharibiwa na watu wasiojulikana.

Bango hilo liliharibiwa baada ya Wakenya mtandaoni kulalamika kuhusu tangazo hilo lililokuwa limeandikwa kila kitu kwa Kichina.

Ni nambari za simu ambazo zilikuwa zimeandikwa kwa herufi za Kilatini ambazo ziliweza kusomeka.

Image caption Mabaki ya bango hilo baada ya kuharibiwa

Wakenya mtandaoni walilalamika ni vipi bango hilo 'lisiloeleweka' na wenyeji liliidhinishwa kuwekwa kwenye barabara hiyo bila kutafsiriwa kwa Kiingereza au Kiswahili.

Baadhi waliwaomba maafisa wakuu serikali wawasaidie kutafsiri:

Mtangazaji huyu alisema matangazo yanafaa kuwa kwa Kiingereza na Kiswahili na kupendekeza liondolewe.

Baadhi hata hivyo walitetea bango hilo wakisema huenda aliyeliweka aliwalenga Wachina pekee.

Miongoni mwa waliolalamika ni Shirikisho la Watumizi wa Bidhaa na Huduma Kenya (Cofek).

Nani aliweka tangazo hilo?

Tangazo hilo liliwekwa na kampuni ya ujenzi ya Yunnan International.

Tangazo hilo lilisema nini?

Tafsiri iliyofanywa na Idhaa ya Kichina ya BBC inaonesha linasema:

Yunnan International

Kituo cha huduma zote za ujenzi

  • Uanakandarasi
  • Masuala ya wafanyakazi
  • Bidhaa za ujenzi
  • Utengenezaji wa bidhaa
  • Utengenezaji wa chuma
  • Huduma za usalama
  • Matangazo
  • Ukarabati na utunzaji
  • Mnara wa maji na uhifadhi wa maji

Nambari ya simu ya moja kwa moja: 0708 848 008

Kampuni ya kuaminika na ya kusifika

Yenye kufanya kazi kwa utaalamu na njia bora zaidi

Huduma ya kiwango na ubora wa juu

Baadhi ya Wakenya mtandaoni waliingiza utani:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii