Kwa Picha: Mlipuko wa volkano 'wameza' nyumba za watu Hawaii, Marekani

Lava consumes a home, as volcanic activity continues on Kilauea"s east rift zone, within the Leilani Estates subdivision, near Pahoa, Hawaii, USA, 06 May 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nyufa zaidi zimetokea katika mitaa ya Leilani na kuharibu nyumba za watu

Milipuko ya volkano katika eneo la Kilauea, Hawaii imeharibu zaidi ya nyumba 26 na inatishia kuharibu nyumba nyingine mamia kadha.

Nyufa mpya zilitokea usiku maeneo hayo. Tayari watu zaidi ya 2,000 wamehamishwa makwao.

Baadhi waliruhusiwa kurejea Jumapili kuokoa wanyama wao, lakini maafisa wa serikali wanasema eneo hilo si salama.

Nyufa na mashimo mapya yalizuka usiku mtaa wa Leilani. Matope yenye moto yalirushwa futi 230 (mita 70) hewani.

Kisiwa hicho kilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 6.9 katika vipimo vya Richter Ijumaa.

Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.

Haki miliki ya picha USGS
Image caption Baadhi ya maeneo, nyufa zinazofuka moshi zilizuka
Haki miliki ya picha USGS
Image caption Matope ya volkano yakirushwa mitaa ya Makamae na Leilan
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wanasema nyumba 26 zimeharibiwa kisiwani humo. Mamia zaidi zimo hatarini
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyufa kumi tofauti zimezuka maeneo ya karibu, eneo la umbali wa 40km kutoka kwenye shimo la katikati ya mlima
Huwezi kusikiliza tena
Matope ya volkano yanaendelea kumwagika kutoka kwa volkano ya Kilauea, Hawaii
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya wakazi waliruhusiwa kurejea kuwachukua wanyama wao baada ya kujaza fomu
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wengi wanaishi kwenye kambi ya muda. Hawajui wataruhusiwa kurejea lini
Haki miliki ya picha USGS
Image caption Volkano ya Kilauea ililipuka Ijumaa, baada ya tetemeko la nguvu ya 6.9
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moshi wa volkano ukifuka kutoka kwa mlima Kilauea
Haki miliki ya picha Getty Images
Haki miliki ya picha Reuters
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.

Soma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii