Utaishi kwa muda gani zaidi duniani?

Umri wa kuishi duniani umekuwa ukiongezeka katika mataifa mbalimbali duniani - na kwa wastani, watu waliozaliwa mwaka 2016 wataishi kwa miaka saba zaidi ya waliozaliwa miaka 25 iliyopita.

Jaza maelezo kukuhusu hapa chini kubaini umri ambao watu wa jinsia sawa na yako kutokana nchini mwako wa umri sawa na wako wanatarajiwa kuishi, na pia ufahamu ni kipindi cha muda gani cha maisha yako unatarajiwa kuwa na afya bora.

Umri wa wastani wa kuishi duniani ni miaka 72 - miaka 70 kwa wanaume na 75 kwa wanawake. Hata hivyo, hili hubadilika kadiri umri unavyosonga. Kwa mfano, mtu aliye na miaka 69 anaweza kutarajia kuishi miaka mingine 17 kwa kiwango cha wastani.

Iwapo unashindwa kufungua kikokotoo hiki, tafadhali bofya hapa kukifungulia.

Kikokotoo hiki hufanya kazi vipi?

Data iliyotumiwa katika kikokotoo hiki inatokana na takwimu za karibuni zaidi (2016).

Umri wa kuishi ni idadi ya miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi kwa kuzingatia umri wake, jinsia na nchi.

'Ni sehemu gani ya miaka uliyosalia nayo itakuwa ya afya' imehesabiwa kwa kutumia idadi ya miaka ambayo mtu anaweza kutarajia akiwa na afya, ambayo inaoneshwa kama asilimia ya umri uliosalia ambao wanatarajiwa kuishi.

Matokeo yanachukulia kwamba viwango vya vifo na ulemavu havitabadilika katika maisha ya mtu.