Mlipuko wa Ebola DRC: WHO lasema Ebola haujafika kiwango cha kutangazwa hali ya dharura

Health workers at Bikoro hospital in DR Congo Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Watu 33 wanajulikana kufariki

Shirika la afya duniani WHO linasema mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo haujafika kiwango cha kutangazwa hali ya dharura inayozusha wasiwasi wa kimataifa.

Katika mkutano huko Geneva ulioitishwa kwa dharura kujadili Ebola katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo - shirika hilo limesema mlipuko wa sasa haijafikia vigezo vya kutangazwa hali ya hatari na halikupendekeza vizuizi vyovyote vya usafiri wala biashara.

Kamati ya muongozo wa kimataifa ya shirika hilo hatahivyo imesema kuna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na aina ya mlipuko wa sasa wa Ebola DRC.

Kumetokea milipuko kadhaa katika maenoe ya mashinani na maeneo ambayo sio rahisi kuyafikia.

WHO linasema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamkaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.

Limeeleza kuwa watu hao wanatizamwa kwa makini na huenda watakuwa miongoni mwa wau wa wa kwanza watakaopewa chanjo ya majiribio ya Ebola.

Kuliripotiwa visa kadhaa katika eneo la mashinani huku kisa kimoja kikithibitishwa katika mji wa

Mji huo ulio na takriban watu milioni moja ni eneo kuu la usafiri katika mto wa Congo, hali inayozusha wasiwasi kwamba huedna virusi hivyo vikasambaa zaidi, na kutishia mji mkuu Kinshasa na nchi jirani.

Ebola ni ugonjwa unaoambukiza unaosababisha kuvuja damu ndani ya mwili na mara nyingi waathiriwa hufariki.

Unaweza kusambaa kwa haraka kwa kugusa maji maji yanayotoka mwilini mwa muathiriwa, na mara nyingi dalili za kwanza za ugonjwa huo zilizo kama homa ya kawaida siyo rahisi kuzitambua.

WHO awali lilikiri kwamba lilichukuwa muda mrefu kukabiliana na janga la Ebola katika Afrika magharibi kati ya 2014-2016.

Mlipuko wa Ebola wa mwaka 2014-16 Afrika uliowaua watu 11,300 ulikuwa mbaya zaidi kwa sababu ulisambaa kwenda miji mikuu ya nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia

Afisa wa cheo cha juu wa shirika la afya duniani (WHO) Peter Salama alisema kusambaa kwa ebola kwenda Mbandaka kunamaanisha kuwa huenda kukawa na visa vya milipuko ya ugonjwa huo.

Ni hatua gani inachukuliwa kudhibiti mlipuko huo?

Visa vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo vimerekodiwa sehemun tatu kwenye mkoa wa Equateus, kwa mujibu wa WHO.

Wafanyakazi wa afya wametambua watu 430 ambao huenda wakikarbiana na ugonjwa huo na pia wanajaribu kuwatafuta wengine 4000 ambao wametawanyika kwenda kaskazini magharibi mwa Congo.

Wengi wa watu hawa wako maeneo ambayo yanaweza kufikiwa na watu kwa kutumia pikipiki.

Siku ya Jumatano dawa ya majaribio ya ugonjwa wa ebola iliyotumwa na WHO iliwasili nchini humo huku nyingine ikitarajiwa kuwasili hivi karibuni.

Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016, Ebola inaaminiwa kusambazwa maeneo ya mbali na popo na mara nyingi husambaa kwenda kwa binadamu kupitia nyama ya msituni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dawa ya majaribio imewasili DRC

Pia unaweza kusambaa kwenda kwa binadamu kwa njia ya damu au viungo au majimaji ya mwili kutoka kwa wanyama walio ugonjwa huo. Hao ni pamoja na sokwe, tumbili na swara.

Ugonjwa huo husambaa kwa haraka na sio rahisi kumaliza wanyama wote wanaoweza kuwa nao. Ikiwa binadamu watakaribiana na wanyama hao kawaida kuna uwezekano kuwa Ebola unaweza kurudi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii