Paul Ogalo: Kasisi anayetumia nyimbo za kufoka kuwavutia vijana Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Paul Ogalo: Kasisi anayetumia nyimbo za kufoka kuwavutia vijana Kenya

Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki nchini Kenya Paul Ogalo a.ka ‘Sweet Paul’ anatumia muziki wa kufoka kama njia ya kuwavutia vijana kufika kanisani.

Anasema aliona muziki kuwa njia mwafaka sio tu kuwavutia vijana bali pia kueneza Injili.

Kwa sasa anaandaa albamu mpya ya muziki wa kufoka na ana matumaini ya kufanya kazi na wasanii wa Kenya na Tanzania akiwemo Bahati, Wyre na Nameless na nyota wa muziki kutoka Tanzania Diamond.

Video: Anthony Irungu, BBC

Mada zinazohusiana