Wafuasi wa Ibori waleta ghasia Nigeria

James Ibori
Image caption Bw Ibori alikuwa gavana nchini Nigeria.

Polisi waliokuwa wakijaribu kumkamata aliyekuwa gavana nchini Nigeria kwa madai ya kuhusika na ufisadi ameshambuliwa na wafuasi wake.

Maafisa wa polisi wameshambuliwa Oghara, mji anapoishi James Ibori lililopo kwenye jimbo la Delta.

Bw Ibori ameshutumiwa kuhusika na ufisadi na ubadhirifu wa fedha akiwa madarakani na tume ya uchumi na fedha ya nchi hiyo, EFCC.

Siku ya Jumanne, mkuu wa polisi aliamuru kukamatwa kwa Bw Ibori katika kipindi cha saa 24.

Msemaji wa polisi ameiambia BBC kuwa shambulio hilo halitozuia mamlaka husika kutimiza wajibu wao wa kikatiba wa kumkamata Bw Ibori.

Siku ya Jumatatu, wafuasi wa Bw Ibori waliweka vizuizi kwenye barabara inayoelekea Oghara kupinga madai ya tume hiyo dhidi ya Bw Ibori.