Rooney kurejea uwanjani

Wayne Rooney na Rio Ferdinand wamefanya mazoezi na kikosi cha United siku ya Ijumaa, kabla ya mechi dhidi ya Sunderland Jumamosi.

Gary Neville ambaye ametia saini mkataba mpya, hana uhakika sana wa kuanza kutokana na kuwa majeruhi.

Image caption Wayne Rooney amefanya mazoezi Ijumaa

Sunderland hawatokuwa na mlinzi wao Allah Hutton ambaye anatumukia adhabu ya kadi nyekundu, na hivyo nafasi yake huenda ikachukuliwa na Phil Bradsley.

Lee Cattermole na John Mensah wanatazamiwa kurejea, lakini George McCartney na Andy Reid hawatocheza kabisa.