UN waonya juu ya kuondoa majeshi mapema

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ameonya dhidi ya kuwaondosha mapema majeshi ya umoja huo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Image caption Majeshi ya kutunza amani ya Umoja wa Mataifa

Serikali ya Kongo inataka majeshi hayo kuondoka nchini humo ifikapo mwisho wa mwezi Agosti.

Lakini wakati wa mazungumzo eneo la mashariki mwa nchi hiyo, John Holmes amesema mkakati wa kuondosha majeshi hayo lazima ufikiriwe kwa makini.

Amesema majeshi ya Umoja wa Mataifa yalikuwa yanawalinda raia na mashirika ya kutoa msaada.

Bw Holmes, muandaaji wa masuala ya dharaura wa Umoja wa Mataifa, alikuwa akitembelea majimbo matatu ambapo wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu wanapopata tabu nyingi.

'Kuepuka mishtuko iliyokiuka mpaka'

Kampeni ya kijeshi, inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kuwasaka wapiganaji wa Kihutu wa Rwanda wanaojihifadhi mashariki mwa Kongo imewalazimu maelfu ya watu kuhama makazi yao katika miezi michache iliyopita.

Akizungumza siku ya Ijumaa, Bw Holmes amesema muda wa watunza amani hao kuondoka utategemea namna majeshi ya Kongo yalivyojiandaa.

Bw Holmes, ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano nchini humo, amesema ana wasiwasi wa kuondoka ghafla kwa majeshi ya umoja huo, inayojulikana kama MONUC.

Bw Holmes amesema, "Kila mtu anajua MONUC haiwezi kukaa milele."

Serikali ya Kongo imeiomba MONUC kuondoka ifikapo mwisho wa mwezi Agusti mwakani, kabla tu ya uchaguzi wa Rais.

Bw Holmes atajadiliana na Rais Jospeh Kabila juu ya kuwalinda raia siku ya Jumatatu.