Milipuko Somalia yaua takriban 30

Takriban watu 30 wamefariki dunia kutokana na milipuko iliyotokea katika msikiti mkuu kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa katika mlilipuko iliyotokea kwenye soko la Bakara.

Image caption Ndugu wakimbeba mwenzao aliyejeruhiwa kwenye mlipuko Mei mosi 2010.

Ripoti moja iliyotolewa imesema kiongozi mmoja mwandamizi wa wapigananji wa al-Shabab ndiye aliyelengwa. Fuad Mohammed Khalaf, anayejulikana kama Fuad Shongole, ametajwa kujeruhiwa.

Wapigananji hao wenye ushirikiano wa karibu na al-Qaeda, wanapewa sifa ya kuweza kuweka amani na utulivu katika maeneo waliyoyadhibiti Somalia.

Shambulio hilo lililotokea karibu na msikiti wa Abdallah Shideye limefanyika wakati wa swala.

Kukatwa viungo vya mwili

Shahidi mmoja ambaye jina lake halikutajwa ameliambia shirika la habari la Reuters, "Watu wengi waliokuwa wakipiga kelele walikuwa wamepandiana, wengine wakiwa wamekufa, baadhi wamejeruhiwa."

Amesema wengi wamejeruhiwa, na wanamgambo wenye silaha wamefika eneo la tukio.

Msikiti wa Abdallah Shideye aghalabu hutumiwa na wapiganaji wa al-Shabab kutoa hutuba.

Image caption Wapiganaji Somalia

Siku ya Jumanne,bomu la ardhini limemwuua mtu mmoja katika msikiti wa Abu Hureya lilipo eneo hilo hilo.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Marekani, Human Rights Watch limesema kuongezeka kwa usalama katika maeneno yanayodhibitiwa na al-Shabab mwezi uliopita yamewaletea tabu sana watu wa kawaida.

Ripoti hiyo imeelezea mauaji, uonevu na adhabu kali za sheria za kiislamu, likiwemo la kukatwa viungo kwa raia.

Katika miaka ya hivi karibuni, wapiganaji hao wamedhibiti eneo kubwa la kusini mwa Somalia.

Kundi kuu la al-Shabab limesema linapambana na jeshi dhaifu la serikali linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuifanya nchi hiyo iwe taifa la kiislamu.

Serikali ya mpito -inayodhibiti maeneo machache ya mji mkuu wa Mogadishu ikishirikiana na majeshi ya Afrika ya kutunza amani-nayo pia inataka kutii sheria za kiislamu, lakini al-Shabab limekuwa likitafsiri sheria hizo tofauti.