Ubingwa wanukia Chelsea

Chelsea imekaribia kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuichapa Liverpool kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Anfiled.

Image caption Drogba

Didier Drogba ndiye alipachika bao la kwanza baada ya nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kufanya makosa ya kumrudishia kipa wake mpira, ambao Drogba aliukimbilia na kupachika bao la kuongoza. Hadi mapumziko Chelsea ilitoka kifua mbele kwa bao 1-0.

Image caption Chelsea wanaelekea kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya England

Kipindi cha pili kilianza taratibu, na dakika nane tu baada ya mapumziko hayo, Frank Lampard aliandika bao la pili na la ushindi.

Liverpool wakionekana kuchoka kutokana na mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya Atletico Madrid, hawakuonesha dalili zozote za kuzinduka.