Jonathan aapishwa rais mpya Nigeria

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.
Image caption Rais Goodluck Jonathan ana jukumu la kuimarisha utulivu mpaka uchaguzi utakapofanyika mwaka ujao.

Kaimu Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ameapishwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo kutokana na kifo cha Rais Umaru Yar'Adua aliyekuwa akiumwa kwa muda mrefu.

Bw Jonathan, aliyekaimu tangu mwezi Februari, atamteua makamu wake na kuendelea kuongoza mpaka mhula wa madaraka utakapokamilika mwaka ujao utakapofanyika uchaguzi mpya.

Bw Yar'Adua alifariki Jumatano katika mji mkuu Abuja.

Maelfu ya watu walihudhuria mazishi yake kwenye mji alikozaliwa wa Katsina. Nigeria imetangaza siku saba za maombolezo.

Bw Jonathan alikula kiapo mbele ya baraza la mawaziri na maafisa wengine wa serikali mjini Abuja, saa 12 baada ya kifo cha Bw Yar'Adua. Shughuli hiyo ilisimamiwa na Jaji mkuu Alloysius Katsina-Alu.