Kongamano la Machifu wa Kiafrika laanza

Mfalme kutoka jamii moja nchini Ghana akitoa baraka

Ghana inaandaa kongamano la kimataifa linalonuia kuimarisha uhisiano kati ya viongozi wa kijadi wa Afrika na watawala wa kisiasa kama hatua ya kuleta ustawi.{Africa Global Sister Cities Foundation}.

Mkutano huo wa siku tano utahudhuria wa machifu wa kijamii kutoka nchi kadhaa barani Afirika pamoja na wajumbe wa mashirika ya kimataifa.

Mshirikishi wa kongamano hilo Nana Ken Otchere ameambia BBC kwamba watawala wa kijadi huwa na mchango muhimu katika jamii za Kiafirika.

Amesema ushirikiano kati ya machifu na maafisa wa serikali ni muhimu kwa ukuaji wa kijamii na kiuchumi.