Mswada mpya wa mazingira Marekani

Robert Kerry na Joe Liberman wanapendekeza mswada wa mazingira

Maseneta wawili wa Marekani wamezindua mswada muhimu unaolenga kupunguza kutegemewa kwa mafuta kutoka nje na kukabiliana ongezeko la joto duniani.

Mswada huo wa mazingira na kawi unaungwa mkono na seneta John Kerry, mshirika wa karibu wa rais Obama na Joe Lieberman.

Inapendekeza kupunguzwa kwa gesi inayochafua mazingira kwa asilimia kumi na saba ifikapo mwaka 2020.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kutokana na kuvuja kwa mafuta katika ghuba ya Mexico, matumaini ya kupita kwa mswada huu ni madogo.

Nia kuu ya marekani ni kupunguza utoaji wa gesi inayochafua mazingira kwa asilimia kumi na saba katika muda wa muongo mmoja ujao na asilimia themanini kufikia mwaka 2050-ni kazi kubwa kwa vyovyote vile.

Mswada huo unatilia mkazo nguvu za nuklia na teknolojia na makaa safi kwa kutoa fedha. Inalazimisha viwanda na makampuni ya umeme kupunguza utoaji wa gesi inayochafua mazingira.

Wakati wa kuleta mswada huo Seneta wa chama cha Democratic John Kerry anasema ana matumaini kuwa mswada utafikia malengo mengi.

Kinachoshangaza,mswada huo mswada huo unaunga mkono uchimbaji wa mafuta katika mwambao wa pwani ya Marekani,kutokana na kumwagika kwa mafuta hivi majuzi katika ghuba ya Mexico.

Ikulu ya Marekani ya white house imeunga mkono sheria ya kawi ya Marekani,lakini itahitaji kuungwa mkono na maseneta wa chama cha Republican ili kupitishwa na kuwa sheria.