Salva Kirr kuapishwa leo kama rais

Image caption Salva Kirr Rais wa Sudan Kusini

Aliyekuwa kiongozi wa waasi Kusini mwa Sudan Salva Kirr Mayardit, ataapishwa hii leo kama raia wa eneo la Sudan Kusini.

Kirr alishinda kwa idadi kubwa ya kura uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita na kuhifadhi kiti hicho cha urais sawia na hasimu wake wa zamani Omar al Bashir katika uchaguzi wa urais ngazi ya kitaifa.

Uchaguzi huo ni sehemu ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka wa 2005 uliomaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 21.

Januari mwaka ujao raia wa Sudan Kusini watapiga kura ya maoni kuamua ikiwa eneo hilo litajitawala.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema raia wengi wa eneo la Kusini watapiga kura kuunga mkono uhuru wake, ikiwa shughuli hiyo itakuwa huru na wa haki.