Je una picha za Kombe la Dunia?

Image caption Unakaribishwa kutuma picha yoyote inayohusiana na Kombe la Dunia, iwe ni mwaka 2010 au michuano iliyopita.

Kwa mara kwanza barani Afrika, kishindo cha Kombe la Dunia kitasikika. BBC inakualika utuonyeshe michuano hiyo inakugusa vipi, unashabikia timu gani? Huenda ikawa timu yako ya taifa haijawahi kugusa fainali za Kombe la Dunia, lakini inawezekana kuna timu nyingine kipenzi chako.

Tutumie picha kwa njia ya barua pepe na tutazichapisha katika tovuti ya bbc ya kiingereza na kiswahili. Inaweza kuwa fulana ya timu unayoishabikia, ukiwa umeivaa au ikiwa dukani. Au gari lenye nakshi za kombe la dunia. Chochote kuhusu michuano hiyo.

Au tuseme, je utakwenda Afrika Kusini? Maandalizi yamefikia wapi? Unaenda kwa njia gani? Hayo yote yanaweza kuzaa picha nzuri kabisa.

Hakikisha kuwa picha unayotuma haikiuki maadili kwa maana kwamba haina lugha chafu au haimchafulii sifa mtu mwingine.

Unakaribishwa kutuma picha yoyote inayohusiana na Kombe la Dunia, iwe ni mwaka 2010 au michuano iliyopita. Tutumie picha kwa barua pepe na tutazichapisha katika tovuti ya bbc ya kiingereza na kiswahili. Unaweza kutuma picha hizo katika anwani ifuatayo: yourpics@bbc.co.uk (ukurasa wa kiingereza)au tutumie kupitia swahili@bbc.co.uk

Hakikisha kuwa umeandika jina lako, mahali ulipo na maelezo kidogo kuhusu picha yenyewe.

Au ingia hapauweze kuituma kupitia fomu hii. Vile unaweza kutuma picha moja kwa moja kwa kutumia simu ya mkononi kupitia +44 77 25 100 100.