Wapenzi wa jinsia moja kujua hatma yao

Wapenzi wa jinsia moja
Image caption Wapenzi wa jinsia moja

Mahakama kuu nchini Zimbabwe, hii leo inatarajiwa kusikiliza ombi la kuachiliwa kwa wafanyakazi wawili wa shirika la pekee nchini humo linalotetea maslahi ya wapenzi wa jinsia moja waliokamatwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Wawili wao wanatuhumiwa kuhujumu mamlaka ya rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe na pia kumiliki picha za ngono. Ulawiti umeharamishwa nchini Zimbabwe.

Chama cha rais Mugabe cha Zanu-PF, kimesema kinataka mjadala kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja kutengwa na majadiliano yanayoendelea kuhusu katiba mpya mpya nchini humo.