Al Bashir kuapishwa kwa muhula mwingine

Rais Bashir wa Sudan

Rais wa Sudan Omar al Bashir ataapishwa rasmi hii leo kwa awamu nyingine kama rais wa Sudan kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Rais Bashiri anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuhusiana na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Viongozi wengi wa serikali wametangaza kuwa hawatahudhuria sherehe hiyo.

Wafuasi wa rais huyo wanasema marais watano kutoka nchi jirani wamethibitisha kuwa watahudhuria.

Uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita nchini Sudan ulikashifiwa na waangalizi wa kimataifa na vyama vingi vya upinzani vilijiondoa kutoka kwa uchaguzi huo wakidai kuwepo kwa wizi wa kura ya unyanyasaji wa wapiga kura.