Wakili kufikishwa mahakamani Rwanda

Mavuvu ya watu waliouawa nchini Rwanda
Image caption Mavuvu ya watu waliouawa nchini Rwanda

Wakili mmoja wa Marekani leo anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Rwanda kwa tuhuma za kufahamu njama za mauji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.

Wakili huyo Peter Erlinder, ambaye pia anatuhumiwa kwa kukana mauaji hayo, alisafiri nchini humo wiki jana na akipanga kumwakilisha kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire.

Ingabirie anakabiliwa na tuhuma za kuchochea hisisa za mauaji ya kimbari. Lakini waziri wa mambo ya nje Bi Louise Mushikiwabo, amesema kuwa Bw. Erlinder hana idhidni ya kuendesha kazi yake nchini humo na kwamba yuko tu mjini Kigali, kujitangaza na kuendesha kile alichotaja kuwa siasa zake kali.

Kwa mujibu wa waziri huyo, Rwanda imepiga marufuku propaganda kuhusu mauaji ya kimbari, ili kuzuia kutokea tena kwa mauaji kama hayo.