Sarkozy: Mataifa ya Afrika yasipuuzwe

Rais Sarkozy wa Ufaransa
Image caption Rais Sarkozy wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, amesema kuwa anaamini haiwezekani kujadili maswala muhimu duniani bila kuhusisha nchi za Kiafrika.

Ameelezea kuwa ni kosa kubwa kutokuwa na nchi ya Kiafrika ambayo ni mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa rais huyo ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano na viongozi wa Kiafrika unaojadili uhusiano wa kibiashara, maswala ya ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, Ufaransa itajitolea kushinikiza mabadiliko hayo mbele uya mikutano ya nchi 8 zenye ushawishi mkubwa dunaini maarufu kama G8 na pia katika mikutano ya nchi 20 tajiri duniani maarufu kama G20.

Rais Sarkozy aliyasema haya mjini Nice alipokuwa akifungura rasmi mkutano huo unaolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na mataifa ya kiafrika. Nchi 53 zinawakilishwa kwenye mkutano huo.

Madagascar haikualikwa kwenye mkutano huo nayo Zimbabwe ilikataa kutuma ujumbe wake baada ya rais Robert Mugabe kutoalikwa kuhudhuria.