Wawili wafa mashindanoni Rwanda

Ramani ya Rwanda
Image caption Ramani ya Rwanda

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa nchini Rwanda wakati gari lilipopenya kwenye mkusanyiko wa washangiliaji katika mashindano ya magari.

Dereva ambaye ni raia wa Kenya ameripotiwa kupoteza njia alipokuwa akiendesha gari hilo kwa kasi kubwa siku ya Jumapili usiku.

Wawili miongoni mwa waliojeruhiwa wako katika hali mbaya sana.

Mashindano ya magari ya KCB Mountain Gorilla yanayofanywa mashariki mwa wilaya ya Gatsibo yaliandaliwa kusherehekea siku ya mazingira duniani.