Vikwazo vya UN ni upuzi mtupu, Iran

Image caption waandamanji nchini Iran

Iran imepuuzilia mbali vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo na baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa sababu ya mpango wake wa nuklia.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinajad ametaja vikwazo hivyo kama uzembe usio na maana yoyote na kusema kuwa thamani yake ni tambara bovu lililotumika.

Vikwazo hivyo vipya vinaipiga marufuku Iran kununua silaha nzito na kuweka sheria ngumu zaidi za kufanya biashara na mabenki nchini humo.

Image caption waandamanaji nchini Iran

Pia vimeongeza idadi ya viongozi wa nchi hiyo waliopigwa marufuku kusafiri nje. Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa vikwazo hivyo ni hafifu kuliko ilivyotarajiwa na mataifa ya magharibi kutokana an shinikizo za Urusi na Uchina.