Machafuko Kyrgystan. 17 wauawa

Image caption waombolezaji nchini Kyrgystan

Maafisa nchini Kyrgystan wametangaza hali ya hatari nchini humo na kuweka marufuku ya kutoka nje katika mji wa pili wa Osh pamoja na miji mingine iliyoko karibu, kufuatia mapigano yaliyozuka na kusababisha vifo vya watu kumi na saba na kuwajeruhi wengine wengi .

Kwa mujibu wa serikali, vurugu ilizuka kati ya makundi mawili ya vijana wa mtaa na kukithiri kuwa mapigano ya kufyatuliana risasi usiku kucha.

Osh ni mji wa kusini mwa nchi hiyo, na eneo la watu wa kabila la Uzbek, linaloaminika kuwa ngome kuu ya aliyekuwa rais Kurmanbek Bakiyev aliyeng'olewa mamlakani mwezi Aprili.

Image caption machafuko nchini Kyrgystan

Tangu mapinduzi hayo, serikali ya mpito imekuwa na wakati mgumu kudhibiti usalama na sasa kuna wasiwasi wa kuzuka mapigano kati ya makabila ya Kyrgyz na Uzbek.