Kitukuu wa Nelson Mandela afariki dunia

Image caption Kifo cha Zenani Mandela, kimemfanya Mzee Nelson Mandela ashindwe kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Kitukuu wa Nelson Mandela, Zenani Mandela amefariki dunia.

Afisi ya uhusiano mwema katika wakfu wa Nelson Mandela imesema kuwa msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 13, alifariki katika ajali ya barabarani iliyompata akiwa njiani kutoka sherehe za mkesha wa Kombe la Dunia mjini Soweto.

Duru za polisi zimesema kuwa dereva aliyesababisha ajali hiyo amekamatwa.

Huku hayo yakiarifiwa, mechi ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia kuwahi kufanyika barani Afrika itafanyika Ijumaa jioni kati ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico.

Timu 32 zinachuana kuwania kombe hilo baada ya mwezi mmoja na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, hatahudhuria sherehe ya ufunguzi.