Raia waonywa kutizama runinga-Somalia

Wapiganaji wa Kisomali
Image caption Wapiganaji wa Kisomali

Wapiganaji wa Kiislamu nchini Somalia, wamewaonya raia wa nchi hiyo kutotizama kituo huru cha runinga cha Universal, kwa sababu kituo hicho kinaonyesha na kutangaza habari ambazo wanasema zinakiuka sheria za dini ya Kiislamu.

Waasi hao sasa wametoa makataa kwa wafanyabiashara wanaotangaza bidhaa na huduma zao kupitia runinga hiyo, kusitisha mara moja. Kituo hicho cha Universal kilibuniwa miaka mitano iliyopita na ina makao yao mjini London.

Mwezi uliopita wapiganaji hao wa Kiislamu waliamuru kituo hicho kusitisha matangazo yake katika maeneo kadhaa wanayothibiti nchini humo.

Waandishi wa Habari wanasema Kituo hicho cha Universal ni maarufu miongoni mwa raia wengi wa Somalia kutokana na habari zinazopeperusha.