Ruto kujibu madai ya kueneza chuki

Image caption majeruhi katik ahospitali Kenyatta

Waziri mmoja nchini Kenya ameamrishwa kufika mbele ya kamati maalum inayosimamia utangamano wa kitaifa kujibu madai ya kueneza chuki katika kampeni zinazoendelea kuhusu katiba mpya inayopendekezwa.

Waziri huyo William Ruto amekuwa akiongoza kampeni za kupinga katiba hiyo inayopendekezwa.

Kamati hiyo imeelezea wasiwasi kuwa wanasiasa wanatumia kampeni kuhusu katiba hiyo kueneza chuki.

Image caption waziri william ruto

Wasiwasi umeongezeka zaidi baada ya watu 5 kufa na zaidi ya 75 kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea katika mkutano wa hadhara siku ya Jumapili. Tangu kutokea milipuko hiyo kumekuwa na visa vya kulaumiana kati ya wanasiasa na viongozi wa kidini na bado haijulikani ni nani aliyehusika na milipuko. Polisi wameanzisha uchunguzi.