Chama cha SPLM chapewa wizara muhimu

Rais wa Sudan akiwa na wafuasi wake
Image caption Rais wa Sudan akiwa na wafuasi wake

Chama tawala Kaskazini mwa Sudan kimesema rais Omar Al Bashir amemteuwa raia wa eneo la Kusini kama waziri wa mafuta katika jaribio la kuhifadhi umoja wa kitaifa.

Afisa mmoja wa chama tawala cha National Congress Party, NCP, Ibrahim Ahmed Omar, ameiambia BBC kuwa hatua hiyo inanuia kujenga imani baada ya juhudi za hapo awali za kuwahakikishi raia wa eneo hilo la Kusini kuwa mapato ya taifa yanayotokana na mafuta yatagawanywa kwa njia ya haki kushindwa kuzaa matunda.

Amesema chama cha NCP, kinatarajia kuwa uteuzi huo wa raia wa eneo la Kusini kusimamia wizara muhumi, itawashinikiza kupiga kura kupinga kugawanywa kwa taifa hilo mapema mwaka ujao.

Wakati huo huo Baraza jipya la mawaziri wa serikali ya muungano nchini Sudan litaapishwa hii leo.

Baraza hilo lililotangazwa na rais Omar Al Bashir hapo jana lina jumla ya mawaziri 77, 7 kati yao wakiwa wanawake.