Kaimu rais Goodluck kimya kuhusu uchaguzi

Rais Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amakataa kuzungumzia ikiwa atawania kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu nchini humo mwaka ujao.

AKihutubia taifa kupitia kwa televisheni ya kitaifa, Jonathan ameliambia taifa kuwa anasubiri wakati muafaka ili kutangaza uamuzi wake.

Waandishi wa habari wanasema uamuzi wake wa kuwania kiti cha urais, utazua mjadala mkali, kwa sababu anatoka eneo la kusini ambako idadi kubwa ya raia ni waumini wa dini ya Kikristu.

Kwa mujibu wa mkataba ambao haujanakiliwa, popote na chama tawala nchini humo, rais atakaye chaguliwa anapaswa kutoka eneo la Kaskini ambako idadi kubwa ya raia ni Waislamu.

Jonathan alitwaa madaraka ya kuliongoza Nigeria baada ya kifo cha mtangulizi wake, Umaru Yar'Adua, ambaye alitoka k eneo la Kaskazini na alitarajiwa kuwania muhula mwingine kama rais.