Ajali ya ndege msituni Congo haina manusura

Image caption Ramani ya Congo

Maafisa wakuu nchini Congo wamethibitisha kutokuwepo manusura wa ajali ya ndege iliyotokea kati ya msitu wa Congo Brazaville na Cameroun siku ya Jumanmosi.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba wakurugenzi ya makampuni ya madini wengi wakiwa raia wa Australia.

Watu hao akiwemo mfanyabishara na tajiri mkubwa nchini Australia, Ken Talbot walikuwa safarini kutoka Cameroun kuzuru mgodi wa chuma, nchini Congo.

Takriban Maiti wote walipataikana, ingawa waziri wa mambo ya nje wa Australia,itachukua muda kabla ya kuwatambua na kisha kuwarejesha nyumbani maiti.

Kiini cha ajali kingali kujulikana.