Washukiwa wa njama ya kumuua Nyamwasa waachiwa

Image caption Generali wa zamani jeshini Rwanda Kayumba Nyamwasa

Polisi nchini Afrika Kusini wameachilia washukiwa wawili waliokamatwa kufuatia jaribio la kumuua kamanda wa zamani wa jeshi la Rwanda mjini Johannesburg Kayumba Nyamwasa.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi washukiwa wengine wanne waliosalia watafikishwa mahakamani tarehe ishirini na tisa mwezi ujao.

Luteni Generali Kayumba Nyamwasa alikuwa anarejea nyumbani Jumamosi iliyopita wakati alipopigwa risasi tumboni na mtu asiyejulikana.

Bwana Nyamwasa angali anapata nafuu. Mkewe amedai serikali ya Rwanda inahusika na njama ya kumuua generali huyo wa zamani, madai ambayo Rwanda imekanusha.