Mkutano wa IGAD kuhusu Somalia waanza

Wanajeshi wa Somalia
Image caption Wanajeshi wa Somalia

Viongozi wa serikali ya nchi wanachama wa muungano wa IGAD wanaanza mkutano wa dharura muda mfupi ujao mjini Adis Ababa Ethiopia kujadili hali ya kisiasa na kiusalama nchini Somalia.

Viongozi hao wa IGAD wanataka wanajeshi wa umoja wa mataifa kuchukua mahala pa wanajeshi wa muungano wa afrika ambao wameshindwa kuthibiti hali hiyo nchini Somalia.

Vile mkutano huo unatajiwa kushinikiza wafadhili waliokuwa wametoa ahadi ya kuisadia serikali ya Somalia, kutimiza ahadi zao.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa mapendekezo kadhaa ambayo yatawasilishwa kwa mkutano wa wakuu wa vongozi wa serikali wa muungano wa afrika utakaoandaliwa baadaye mwezi huu.