Jeshi la UN yalalamikia serikali ya Sudan

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa
Image caption Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa

Jeshi la kimataifa la kutunza amani nchini Sudan, UNAMID limetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo na wanajeshi wa waasi kuondoa vikwazo vya usafiri katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.

Kiongozi wa jeshi hilo la Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika, Ibrahim Gambari, amesema waasi hao na wanajeshi wa serikali wamewazuia wanajeshi hao wa kutunza amani kuingia maeneo yaliyoshuhudia mapigano makali, miezi ya hivi karibuni.

Gambari amesema vikwazo hivyo vinakiuka sheria za kimataifa kuhusu haki za kibinadamu.