Kombe la Dunia: Mjadala wa kimataifa

Image caption Mazungumzo kuhusu Kombe la Dunia.

Wasimulizi na wachambuzi wa soka kote duniani wamesema waliyosema kuhusu mazuri na mabaya katika michuano ya Kombe la Dunia, lakini mashabiki wana maoni gani, kuhusu ufanisi wa timu zao na timu mwenyeji?

IFIKAPO SAA MOJA ZA AFRIKA MASHARIKI BOFYA HAPA: bbcworldservice.com/worldcupteamtalk

Kama sehemu ya matangazo ya Kombe la Dunia 2010, BBC inataka kuwakutanisha mashabiki kutoka kote duniani kutoa maoni yao hasa kugusia maswala muhimu yaliyotawala Kombe la Dunia - ikiwa ni pamoja na magoli bora, mashabiki bora, mabadiliko waliyofanya makocha na maelezo ya nini kiliwafurahisha au kuwaudhi wakati wa mashindano.

Tutakuwa hewani kuanzia saa moja wa Afrika Mashariki kupitia bbcworldservice.com/worldcupteamtalk, hadhira kutoka dunia nzima itaweza kujumuika katika mjadala na kubadilishana mawazo, bila kukwazwa na vizingiti vya lugha.

Jamvi la ujumbe litafanya tafsiri maoni katika lugha 10 tofauti ikiwa ni pamoja na: Kiarabu, Kialbania, Kichina, Kiingereza, Hispania, Kiajemi, Kireno,Kiswahili, Kivietnam na Kiwelshi, pamoja na tafsiri ya moja kwa moja ya maoni na maswali kwa Kiingereza kuwezesha watu wa lugha nyingine kushiriki katika majadiliano.

Lengo letu ni kuwezesha watu kuona, kusikia na kusoma kile mashabiki kutoka sehemu nyingine duniani wanavyojadili, na kuweza kutazama mazungumzo hayo.

Jumuika nasi kupata uhondo Ijumaa, tarehe 9 Julai 2010, saa moja za Afrika Mashariki.

IFIKAPO SAA MOJA ZA AFRIKA MASHARIKI BOFYA HAPA: bbcworldservice.com/worldcupteamtalk