Kenya yaelezea wasi wasi wa kushambuliwa

Moses Wetangula
Image caption Moses Wetangula

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula, ameonya kuwa wapiganaji wengi wa Kiislamu wanaingia nchini Somali, kwa nia ya kufanya mashambulizi dhidi ya majirani wake, ikiwemo Kenya.

Wetangula amesema kumekuwa na idadi kubwa ya raia wa Afghanistan, Pakistan na kutoka nchi za Mashariki ya Kati wanaoingia nchini Somalia.

Wetangula hata hivyo hajasema ni wapiganaji wangapi wamefanikiwa kufika nchini humo, lakini amesema ni iadi yake ni kubwa kiasi kwamba Kenya pamoja na jamii ya kimataifa imeanza kuwa na wasi wasi.

Amesema hali hiyo inahitaji kushughulikiwa kwa dharura.

Siku ya Jumatatu rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, alionya kuwa taifa hilo lina thibitiwa na kundi la kigadi la Al-Qaeda na makundi mengine ya wapiganaji wa Kiislamu.