Liwalo na liwe, sitajiuzulu - Naoto Kan

Image caption Naoto Kan asema hatajiuzulu

Waziri mkuu wa Japan Naoto Kan amesema kuwa hatajiuzulu licha ya kushindwa kwa serikali yake katika uchaguzi wa bunge la uakilishi.

Matokeo ya awali yameonyesha kuwa serikali hiyo ya mseto imepoteza viti vingi katika uchaguzi huo na hivyo kutoa wasiwasi wa kuhujumiwa na upinzani.

Alilaumu matokeo hayo kwa pendekezo alilotoa awali la kuongeza ushuru wa mauzo nchini humo.

Image caption Naoto Kana asema hatajiuzulu

Mwandishi wa BBC anasema kuwa matokeo hayo yameonyesha changamoto kubwa kwa serikali hiyo iliyochukua madaraka mwaka jana chini ya chama cha Democratic kwa kuahidi mabadiliko ya utawala.