Lubanga kuendelea kusalia Kizuizini ICC

Thomas Lubanga
Image caption Thomas Lubanga

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, iliyo na makao yake mjini the Haque, imefutilia mbali agizo la kumuachilia huru kiongozi wa waasi nchini Congo, Thomas Lubanga.

Mapema mwezi huu, Majaji wa mahakama hiyo walisimamisha kesi dhidi yake na kusema ni sharti aachiliwe huru.

Majaji hao walisema upande wa mashtaka ulikuwa umehujumu kesi hiyo na kwamba kesi hiyo haingelisikilizwa kwa njia huru na haki.

Viongozi wa mashtaka walikata rufaa kupinga uamuzi huo na mahakama hiyo ya ICC sasa imesema Bwana Lubanga atasalia kizuizini hadi rufaa hiyo itakaposikilizwa. Lubanga anatuhumiwa kuwasajili watoto kama wanajeshi wake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo.

Mshukiwa huyo amekana madai hayo.