Raul astaafu Real Madrid

Image caption Raul

Aliyekuwa mshambuliaji mashuhuri wa Hispania Raul Gonzalez ametangaza kuiacha klabu ya Real Madrid baada ya kuichezea kwa miaka 18 akidai kwamba huenda akahamia klabu ya ligi ya Primia ya England.

Raul mwenye umri wa miaka 33-alitazamiwa kujiunga na klabu ya Ujerumani ya Schalke kwa mkataba wa miaka miwli lakini alikanusha kuwepo kwa mkataba wowote.

Raul amefunga mabao 323 katika mechi 741 alizoichezea Real Madrid na mabao 44 katika mechi 102 alizozichezea Hispania.

Mbali na klabu ya Bundesliga ya Schalke kumekuweko tetesi kwamba klabu za England kama Tottenham, Newcastle, Liverpool na Manchester United nazo pia zinamwangaza Raul.