200 kufikishwa mahakamani Nigeria

Mamlaka nchini Nigeria zinasema zitafikisha mashirika, taasisi na watu binafsi wapatao 260, katika mahakama maalum kuhusiana na shughuli zinazokwenda kinyume cha sheria katika soko la hisa la nchi hiyo.

Image caption Farida Waziri, mkuu wa Tume ya makosa ya kifedha na kiuchumi Nigeria

Washukiwa hao hawajatajwa bado, lakini ni pamoja na madalali wa hisa, wahasibu na wanasheria.

wanashukiwa kwa kufanya uhalifu wa kifedha kama vile kupanga bei za vitu, kupanga hila za kubadili bei za hisa, udanganyifu na kufanya biashara ndani kwa ndani.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema janga la kifedha lililotokea mwaka jana, lilifichua ukiukwaji wa utaratibu katika masoko ya mitaji.

Mwandishi wa BBC anasema kuteuliwa kwa mratibu mpya wa maswala ya kifedha mapema mwaka huu, kumebadili hali ya kifedha ya Nigeria duniani kote.