Nigeria yatinga fainali

Timu ya akina dada ya Nigeria imefuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 huko Ujerumani, baada ya kuishinda Colombia 1-0 katika nusu fainali.

Nigeria imekuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufika hatua ya fainali, na sasa inasubiri kukutana na Ujerumani kwenye fainali kuwania kombe hilo.

Nigeria ilifunga bao la mapema kupitia Ebere Orji katika dakika ya 2.

Ujerumani ilifuzu kwa fainali baada ya kuifunga Korea Kusini 5-1.