United yainyuka Chelsea ngao ya hisani

Chelsea v United
Image caption Chelsea na Man United wamepambana

Manchester United imeichapa Chelsea kwa magoli 3-1 katika mchezo wa kuashirika kuanza kwa ligi kuu ya England.

Mchezo wa ngao ya Hisani huchezwa wiki moja kabla ya kuanza rasmi kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.

Image caption Berbatov

Manchester United waliandika bao lwa kwanza katika dakika ya 41 kupitia mchezaji wake Antonio Valencia baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Wayne Rooney.

Bao la pili limefungwa na mchezaji mpya wa United Havier Hernandez 'Chicharito' katika dakika ya 72 kufuatia krosi ya Antonio Valencia.

Image caption Salomon Kalou

Chelsea walizinduka katika dakika ya 83 na kupachika bao lao kupitia Salomon Kalou, kufuatia kipa wa Man United, Edwin van Der Sar kutema shuti la Daniel Sturridge.

United waliizamisha meli ya Chelsea katika dakika ya 90 kupitia goli lililofungwa na Dimitar Berbatov.