Kura ya maoni ifanyike ilivyopangwa

Image caption Pagam Amum - Kura ya maoni Sudan

Serikali ya Sudan Kusini imelaani mpendekezo kwamba kura ya maoni kuhusu kujitenga kwa eneo lao iahirishwe.

Waziri wa amani katika serikali ya Sudan kusini Pagan Amum, ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha waasi wa zamani wa SPLM, amesema pendekezo lolote la kuahirishwa kura hiyo ya maoni, litakuwa ni uvunjaji wa makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenye vya nchi hiyo.

Takriban wajumbe wawili a tume ya kura ya maoni wametoa wito wa kuahirishwa kwa muda kwa kura hiyo.

Bwana Amum amesema kwamba chini ya mkataba wa amani, serikali ya Sudan kusini inaweza kujiandalia uchaguzi yenyewe kama inawezekana.