UN waitaka Sudan iruhusu misaada

John Holmes
Image caption John Holmes

Mratibu Mkuu wa huduma za misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa, John Holmes, ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuruhusu mashirika ya misaada kuzuru kambi ya wakimbizi iliyoko kusini mwa Darfur.

Bw Holmes alisema wafanyakazi wa mashirika ya misaada hawawezi kuwapatia msaada zaidi ya wakimbizi elfu thamanini wa Darfur katika kambi ya Kalma, kufuatia maandamano yaliyoambatana na ghasia katika eneo hilo wiki mbili zilizopita.

Serikali ya Sudan imekanusha kuweka vikwazo vyovyote ambavyo vinawafanya wafanyakazi wa mashirika ya misaada kutoweza kufika kwenye kambi hiyo.

Bw Holmes alisema maelfu ya wakimbizi kwa hivi sasa hawajulikani walipo na kuonya kuwa kuna hatari ya hali kuzorota kwa haraka.