Albino: Mkenya mahakamani Tanzania

Albino wamekuwa wakiuawa Tanzania kwa imani za kishirikina
Image caption Albino wamekuwa wakiuawa Tanzania kwa imani za kishirikina

Raia mmoja wa Kenya anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Tanzania hii leo kujibu mashtaka yanayomkabili ya kujaribu kumuuza albino mmoja kutoka Kenya.

Polisi nchini Tanzania wamedokeza kuwa mtuhumiwa, Nathan Mutei, alijaribu kumuuza mtu huyo kwa maafisa wa polisi waliojifanya wafanya biashara kwa thamani ya zaidi ya dola laki mbili unusu.

Wamesema Mutei alimhadaa albino huyo Mkenya kuenda naye Tanzania kwa ahadi ya kumpatia kazi.

Tanzania imeshuhudia visa vingi vya mauaji ya albino.

Baadhi ya waganga wa kienyeji wamedaiwa kutumia viungo vya miili ya albino kwa imani za kishirikina wakidai kwamba vitawasaidia wateja wao kupata utajiri au mali.