Mafuriko yaathiri Uchina na Korea Kaskazini

Mto Yalu uliosababisha mafuriko
Image caption Mto Yalu uliosababisha mafuriko

Shirika la habari la Korea ya Kaskazini limesema zaidi ya watu elfu tano wamehamishwa kutoka mji wa Sinuiju kariba na mpaka wa Uchina kufuatia mafuriko makubwa.

Shirika hilo lilisema kuwa kiongozi wa nchi Kim Jong-il aliamuru vikosi vya jeshi kusaidia operesheni za uokozi.

Taarifa kutoka Uchina zinasema kuwa watu elfu tisini na nne wameachwa bila makao katika mji wa Dandong nchini Uchina, ambako kiasi cha nyumba mia mbili ziliporomoka.

Maafisa wa serikali ya Uchina walisema mvua inatarajiwa kuendelea kote katika jimbo hilo hadi siku ya Jumatatu.

Maporomoko ya ardhi na mafuriko yamewauwa zaidi ya watu elfu moja na mia tano kote Uchina katika miezi ya hivi karibuni.