Afisa wa jeshi akamatwa Rwanda

Ramani ya Rwanda
Image caption Ramani ya Rwanda

Serikali ya Rwanda imemtia mbaroni afisa wa jeshi la taifa la nchi hiyo ambaye ni ndugu wa afisa wa zamani katika jeshi la nchi hiyo.

Ndugu huyo, Lieutenant Colonel Rugigana Ngabo, alichukuliwa nyumbani kwake katika mji mkuu, Kigali, na maafisa wa ujasusi wa Rwanda siku ya Alhamis.

Msemaji katika jeshi la serikali ya Rwanda amesema kuwa afisa huyo mwenye mwenye cheo la Luteni kanali ,aliyekamatwa nyumbani kwake mjini Kigali siku ya Al-hamis, alikuwa anajihusisha na vitendo vya uasi wa kisiasa.

Luteni kanali Jill Rutaremara aliliambia gazeti la the New Times nchini humo kuwa Bw Ngabo alihusika na vitendo vinavyohatarisha usalama, na kwa ajili hiyo anashikiliwa na jeshi.

Familia yake inaarifiwa kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wake.

Mr Ngabo ni ndugu yake Generali Faustin Kayumba Nyamwasa aliye uhamishoni, ambaye alijeruhiwa mwezi June nchini Afrika Kusini katika kile kilichoonekana kama jaribio la mauaji.

Nyamwasa alipigwa risasi wakati Rwanda ikijandaa na uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu.