Mahujaji wa Nigeria wazuiwa kwenda Hija

Filamu inayoangazia hija

Ghadhabu kali imezuka Nigeria baada ya Saudi Arabia kutangaza kudhibiti idadi ya raia watakaokubaliwa kufanya hija.

Balozi wa Saudia nchini Nigeria Khalid Abdu Raboh ameiambia BBC kwamba kwanzia mwaka huu mahujaji watakubaliwa kufanya hija mara moja pakee kwa miaka mitano.Balozi huyo amesema masharti haya yametolewa kwa sababu za kiusalama.

Kwenye hija ya awali msongamano wa mahujaji ulisababisha ajali na kupelekea vifo vya mamia ya watu.Ingawa waumini wa Kiisilamu wanatakiwa kufanya hija moja katika maisha yao, mabwenyenye wa Nigeria wamekuwa wakifanya Hija kila mwaka.

Serikali ya Nigeria imependekeza sharti la sasa kuondolewa ikisema wengi wa walionuia kufanya Hija mwaka huu wamepata tiketi zao.